Ugali, mlenda and dagaa (Dry Salted Anchovies, Okra and Ugali)

Nani hatapenda kula ugali na mlenda jamani? Yes, jumatatu nilikula ugali, mlenda na dagaa (dry salted anchovies)


Mlenda 

Sijui hii inastahili kuitwa mlenda kwa wale watu wa Tabora na Mwanza lakini kwangu hii ilikua safi kabisa.

Mahitaji
Mchicha mchanga (Baby spinach)
Bamia
Chumvi
Accent flavor enhancer

Olive oil au veritable oil
Maji 

Directions
Osha bamia na mchicha, kisha zikatekate.
Katika safuria nzito weka kila kitu na funika. Pika katika moto wa medium lakini hakikisha unakoroga kila dakika kadhaa au ukiona mapovu yanapanda juu. Zikishaiva pondaponda jinsi unavyopenda.

Dry Salted Anchovies sauce
Dagaa (Dry salted Anchovies)
Kitunguu
Nyanya
Vegetable oil
Pilipili zilizokaushwa 

Jinsi ya kutengeneza
Ondoa vichwa 
Zioshe kwa maji ya moto halafu ziroweke kwenye maji kama saa moja hivi.
Zikaushe maji na uziwekek pembeni
Weka mafuta kwenye kikaangio chako yakishapata moto weka kitunguu.
Kaanga kikishakua cha brown weka nyanya, chumvi na pilipili
Kaanga mpaka nyanya imelainika 
Weka dagaa
Punguza moto na upike mpaka dagaa zimeiva. Kama nyanya yako ilikua kavu na haikuwa na maji mengi basi ongeza maji kidogo sana ya kutosha kuziivisha tu.


Ugali 
Maji
Unga wa mahindi (White Corn Meal)


No comments: