Jinsi ya Kutengeneza Kachori

Mahitaji

1 pound nyama ya kusaga
5 - 6 viazi ulaya 
2 vijiko vya chakula mafuta ya kupikia
1 kijiko kidogo cha chai cumin powder
1 kijiko kidogo cha chai coriander powder
2 pilipili mbuzi
1 tangawizi
¼ kijiko cha chai garam masala
2 vijiko vya chakula maji ya limao au ndimu
 Pinch chumvi upendavyo
1 kijiko cha chai kitunguu swaumu
5 mayai ya kuku
Mafuta kwa ajili ya kukaanga

Jinsi ya Kutengeneza 
Chemsha viazi kwenye sufuria vikiwa na maganda yake.

Weka nyama ya kusaga, kitunguu swaumu na malimao na  kuikaanga mpaka maji yaishe. Halafu weka maji kidogo kidogo na kuichemsha mpaka iive. Weka pembeni.

Menya viazi ulivyochemsha kisha kata katika vipande vidogo. 

Pasha mafuta ya kupikia kijiko kimoja kwenye kikaango.

Weka cumin, coriander powder, pilipili, tangawizi halafu weka chumvi na viazi. 

Kaanga kwa dakika 2-3 itakua imeiva vizuri.

Ponda mchanganyiko wako mpaka uwe laini kabisa

Chukua mchanganyiko huo wa viazi na tengeneza maumbo madogo ya mviringo ukubwa kama limao kisha bonyeza kwa kutumia kidole kati kati ya umbo hilo utapata nafasi ya kuweka kijiko kimoja cha chai nyama ya kusaga iliyoiva kisha funika kwa kutumia viazi na jitaidi kuviringisha tena kwa kutumia mikono yako miwili ili upate umbo zuri.

Piga mayai pembeni kwenye bakuli na chovya umbo moja moja na weka kwenye kikaango chenye mafuta ya moto kaanga ukishapata rangi tu ya kahawia toa.

Chicken Fowl Soup (Sopu ya Kuku wa Kienyeji)



Mahitaji
Kuku wa kienyeji
Vitunguu
Celery
Giligilani
Limao
Pilipili manga
Chumvi

Homemade Chocolate Chips Banana Muffins (Muffins za Chocolate Chips na Ndizi za Kutengeneza Nyumbani)



Mahitaji
Ndizi
Unga
Chocolate Chips
Baking powder
Baking soda
Sukari
Vegetable oil
Yai
Vanilla extract

Beef Pumpkin Potatoes Soup (Soup ya Nyama ya Ng'ombe, Maboga na Viazi Mviringo)



Nyama
Boga
Viazi mviringo
Vutunguu 
Mchuzi mix
Chumvi

Kama huna mchuzi mix (bullion) tumia viungo vingine ulivyo navyo nyumbani. 

Jinsi ya Kupika Mchuzi wa Kuku na Nazi (Chicken Coconut Stew)



- Mahitaji
- Kuku breast
- Nazi kopo moja/ Cream ya nazi moja
- Biringanya moja
- Viazi mviringo vitatu
- Pilipili Manga kijiko cha chai kimoja
- Chumvi
- Vitunguu
- Vitunguu saumu
- Mafuta ya kupikia
- Limao

Jinsi Ya Kupika
1. Weka viazi kwa sufuria na mafuta. Kaanga mpaka vile brown.
2. Osha nyama na katakata na kuiweka kwenye viazi. Kaanga mpaka iwe brown kidogo.
3. Weka limao na vitunguu saumu endelea kugeuza geuza. 
4. Weka vitunguu na kaanga.
5. Weka biringanya na funika hadi ziive tia kama haina maji basi ongeza kidogo. 
6. Weka vitu vingine vyote kasoro nazi. 
7. Baada ya kuona viazi na nyama imeiva weka  nazi  na pika kwa dakika  5.

Toa jikoni na unaweza kusubiri dakika 5 au 10 kabla hujatumia. Ni nzuri kwa wali, viazi na ugali.

Goat Head Pepper Soup (Supu ya Kichwa cha Mbuzi na Pilipili)


Suou ya kichwa mbuzi ni nzuri sana hasa wakati wa baridi ila siobya kuzoea  kunywa sana kwa vile ina mafuta mengi sana tu.

Mahitaji
Kichwa cha mbuzi
Chumvi
Limao
Pilipili
Pilipili manga
Tangawizi
Celery 
Giligilani
Kitunguu

Changaya kila kitu kasoro giligilani na uichemshe na moto wa kati kwa masaa mawili. Ongeza maji kila unapoona yanaisha. Kama mbuzi ni changa saa moja na nusu inaweza kuwa imeiva tayari. 

Weka giligilani na endelea kuiacha ichemke kwa dakika kumi. Iache ipoe kidogo kabla hujaiweka kwenye bakuli.

Enjoy 

Making Fish and Asparagus on an Air Frier

I am hooked. I love how the food comes out with no oil. The fish is still crispy on the outside and moist inside. The asparagus came out perfect too and crunchy.

Making Crispy Yummy Chicken Wings Using the Air Frier

I was late in the game but so far so good. Love everything about it. 

How to make crispy wings.
Mix in a bowl onion powder, garlic powder, ginger powder,, cumin powder, smocked paprika, chilli powder, black pepper and salt. 

Then mix 1 cup of flour and 1 teaspoon of cornstarch in a tray but you can get crispy wings without the cornstarch. I like this way.

Dry the wings with a paper towel and then mix thoroughly with the onion, garlic mixture. 

Dip your wings in the flour and cornstarch mixture to cover them.. Once they are all covered with the flour arrange them on the rack and follow your air frier instructions for making Chicken Wings. 

Enjoy

Samaki wa Kuoka (Sangara wa Kuoka) (Shake and bake)

Hii ni rahisi sana kutengeneza. Weka samaki  kwenye ndimu au limao na kumuweka kwenye fridge kwa zaidi ya saa moja mpaka sita. 

Chukua chenga za mkate (bread crumbs) na kuweka kwenye mfuko wa plastic. Changanya spices na chumvi kwenye mfuko.  Inapendeza zaidi ukiweka herbs. Halafu unaondoa maji kwa samaki na kupanguza kidogo. Dumbukiza samaki kwenye mfuko na hakikisha unashake mpaka viungo vinaingia samaki wote. 

Weka kwenye chombo cha kuoka ulichopaka mafuta chini. Okay kw dakika 12 hadi 20 inategemea ukubwa wa samaki yako. Ila hakikisha ukichomeka umma  inajitenganisha. 


Bagia za Viazi

Baghia au Bhagia au Bajia su Bajji. Yote ni majina yake. Hizi nimetengeneza kwa kuweka viazi katikati.