Jinsi ya Kupika Mchuzi wa Kuku na Nazi (Chicken Coconut Stew)



- Mahitaji
- Kuku breast
- Nazi kopo moja/ Cream ya nazi moja
- Biringanya moja
- Viazi mviringo vitatu
- Pilipili Manga kijiko cha chai kimoja
- Chumvi
- Vitunguu
- Vitunguu saumu
- Mafuta ya kupikia
- Limao

Jinsi Ya Kupika
1. Weka viazi kwa sufuria na mafuta. Kaanga mpaka vile brown.
2. Osha nyama na katakata na kuiweka kwenye viazi. Kaanga mpaka iwe brown kidogo.
3. Weka limao na vitunguu saumu endelea kugeuza geuza. 
4. Weka vitunguu na kaanga.
5. Weka biringanya na funika hadi ziive tia kama haina maji basi ongeza kidogo. 
6. Weka vitu vingine vyote kasoro nazi. 
7. Baada ya kuona viazi na nyama imeiva weka  nazi  na pika kwa dakika  5.

Toa jikoni na unaweza kusubiri dakika 5 au 10 kabla hujatumia. Ni nzuri kwa wali, viazi na ugali.

No comments: