Suou ya kichwa mbuzi ni nzuri sana hasa wakati wa baridi ila siobya kuzoea kunywa sana kwa vile ina mafuta mengi sana tu.
Mahitaji
Kichwa cha mbuzi
Chumvi
Limao
Pilipili
Pilipili manga
Tangawizi
Celery
Giligilani
Kitunguu
Changaya kila kitu kasoro giligilani na uichemshe na moto wa kati kwa masaa mawili. Ongeza maji kila unapoona yanaisha. Kama mbuzi ni changa saa moja na nusu inaweza kuwa imeiva tayari.
Weka giligilani na endelea kuiacha ichemke kwa dakika kumi. Iache ipoe kidogo kabla hujaiweka kwenye bakuli.
No comments:
Post a Comment