Showing posts with label Snack. Show all posts
Showing posts with label Snack. Show all posts

Samaki wa Kuoka (Sangara wa Kuoka) (Shake and bake)

Hii ni rahisi sana kutengeneza. Weka samaki  kwenye ndimu au limao na kumuweka kwenye fridge kwa zaidi ya saa moja mpaka sita. 

Chukua chenga za mkate (bread crumbs) na kuweka kwenye mfuko wa plastic. Changanya spices na chumvi kwenye mfuko.  Inapendeza zaidi ukiweka herbs. Halafu unaondoa maji kwa samaki na kupanguza kidogo. Dumbukiza samaki kwenye mfuko na hakikisha unashake mpaka viungo vinaingia samaki wote. 

Weka kwenye chombo cha kuoka ulichopaka mafuta chini. Okay kw dakika 12 hadi 20 inategemea ukubwa wa samaki yako. Ila hakikisha ukichomeka umma  inajitenganisha. 


Bagia za Viazi

Baghia au Bhagia au Bajia su Bajji. Yote ni majina yake. Hizi nimetengeneza kwa kuweka viazi katikati.