Kitowewo cha Kuku, Viazi Vitamu na Karanga (Sweet Potatoes, Chicken and Peanut Sauce)


Inatojekea West Africa

Enjoy.

Mahitaji
Kilo moja ya nywama. (ukipata kuku wa kienyeji ni vizuri zaidi)
Vijiko vitatu vya mafuta ya kupikia ya maji
Kitunguu kimoja kikubwa kilichokatwakatwa
Tangawizi kpande kimoja menye na kusaga
Kitunguu saumu kidogo kimoja. Menya na kusaga
Kilo moja ya viazi vitamu vilivyomenywa na kukatwa vipande vipande
Nyanya kubwa mbili zilizomenywa na kukatwa katwa

 
Vikombe viwili vya karanga iliyokaangwa na kupondwa pondwa
Robo kikombe au nusu cha majani ya giligilani yaliyokatwakatwa
Kijiko kimoja cha chai pilipili ya unga kama unapenda
kijiko kimoja cha chai chumvi
Kijiko kimoja cha chai pilipili manga


Jinsi ya kutengeneza

1. Kama unatumia kuku wa kienyeji, chemsha mpaka Iive.

2. Chukua safuria kubwa weka mafuta kwenye safuria mpaka yapate moto, chukua vipande vya kuku uvikaange mpaka viwe vya brown. Vitoe uviweke pembeni.

3. Kwenye hiyo hiyo safuria kaanga vitunguu mpaka viwe vya brown, weka vitunguu saumu navyo vikiivya changanya tangawizi koroga kidog halafu weka viazi vitamu. Kaanga kidogo angalia visiungue.

4. Changanya vitu vyote vilivyobakia kasoro plipili ya unga, pilipili manga na bakiza kama kijiko kimoja cha giligilani ka ajili ya kupamba. Kama ulitumia kuku wa kisasa basi engeza maji au chicken broth kama unayo. kam ulitumia kuku wa kienyeji basi tumia ile supu ya kuku kuivisha kitoweo chako. Punguza moto uchemshe kwa dakika tisini au mpaka viazi viive.

5. Toa nyama na uiache ipoe halafu uitoe mifupa na ngozi yote kama unataka

6. Rudisha kwenye jiko uangalie kama chumvi imetosha , weka pilipili ya unga kama unapenda na pilipili manga jinsi unavyopenda. Hiki kitowewo kinatakiwa kiwe na ladha ya kuwasha. Hivyo weka pilipili manga nyingi kidogo.

No comments: